>

YANGA INAUWAZA UBINGWA

BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Yanga ameweka wazi kuwa mipango ya timu hiyo kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Yanga ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 7 na imekusanya jumla ya mabao 12 ambayo yamefungwa na timu hiyo.

Safu ya ulinzi imekuwa imara ambapo imeokota mabao mawili katika nyavu zake kwenye mechi hizo ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting na Namungo FC.

Mwamnyeto amesema:”Tunahitaji kufanya vizuri na imani yetu ni kuona kwamba mechi zetu zijazo tunashinda ili kupata pointi tatu muhimu.

“Ushindani ni mubwa kwa kuwa kila timu inahitaji kufanya vizuri hivyo kikubwa ni kuzidi kupambana kwa kila mmoja na tuna amini kwamba matokeo mazuri yanakuja,”.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Desemba 11,2021 Uwanja wa Mkapa.