KIUNGO Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Bernard Morrison ameanza kujihami na changamoto za kubambikiwa kesi ya kukutwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Morrison ameonesha hali hiyo kwa kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagarm inayomuonesha akiwa Uwanja wa Ndege, amevaa Barakoa hadi machoni.
Morisson ameandika: Trying to protect myself before they say I have covid in Zambia? #safetyfirst
(Najaribu kujikinga kabla hawajasema nina maambukizi ya vya Virusi vya Corona nikifika Zambia.)
Morrison alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza dhidi ya Red Arrows, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam huku bao lingine likifungwa na Mshambuliaji Meddie Kagere.
Tayari kikosi cha Simba kipo Zambia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa kesho,Desemba 5.