Home International MANCHESTER UNITED YAITULIZA ARSENAL

MANCHESTER UNITED YAITULIZA ARSENAL

USHINDI wa Manchester United wa mabao 3-2 dhidi ya Arsenal umemfanya Kocha Mkuu, Ralf Rangnick kusema kuwa matumaini yake makubwa ni kuona timu hiyo inakuwa kwenye mwendelezo wa ushindi.

Ni Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta alikuwa wa kwanza kushuhudia wachezaji wake wakijaza bao kimiani ilikuwa ni kupitia Emile Smith Rowe dakika ya 13 na liliwekwa usawa na Bruno Fernandes dakika ya 44.

Kipindi cha kwanza ubao wa Old Trafford ulikuwa unasoma United 1-1 Arsenal na kipindi cha pili mambo yalizidi kupamba moto ambapo Cristiano Ronaldo aliwatungua Arsenal dakika ya 52.

Iliwachukua Arsenal dakika mbili kusawazisha bao hilo kupitia kwa Martin Odegaard dakika ya 54 na kuweka usawa katika mchezo huo.

Shujaa alikuwa ni Ronaldo ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 70 kwa penalti na kufanya pointi tatu kubaki ndani ya Uwanja wa Old Trafford.

United ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 14 na Arsenal ipo nafasi ya tano na pointi 23.

Previous articleSALAH ACHEKA ISHU YA BALLON D’OR
Next articleSNURA AZINDUA EP YAKE, AMZUNGUMZIA SHILOLE