>

SNURA AZINDUA EP YAKE, AMZUNGUMZIA SHILOLE

 

MALKIA wa Muziki wa Singeli Snura Mushi a.k.a Snura Majanga ameweka wazi kuwa bado hatamani wala kufikiria kumshirikisha Msanii mwenzake wa bongofleva Shilole.

 

Akizungumza mara baada ya kutambulisha rasmi EP yake ambayo imebeba takribani nyimbo 5 ikiwemo Jini,naota,Kaliamsha, pamoja na Zaina Huku akisindikiza na Kaliamsha yenye maadhi ya Mtindo wa kisasa “Amapiano”.

Hata hivyo Snura amefafanua zaidi kuwa amejipanga vizuri na kwa sasa anafikiria zaidi kujfanya kazi na watu waliomzidi kikazi hivyo hategemei wala kufikiria kufanya kazi na Shilole kwani amemzidi kiuwezo.

Pia ameeleza kwa namna gani ameweza kuufikisha Muziki wa singeli nje ya nchi na kuona kwa jinsi gani baadhi ya Wasanii na watayarishaji wa Muziki kutoka nje na kumtaja Don jazzy kukubali Muziki huo wa Singeli.

 

Aidha, Snura amesema ndani ya Ep yake imebeba mafunzo mengi yenye kufundisha na kuelimisha hivyo amewataka mashabiki kuendelea kumpa ushirikiano wakutosha katika kupakua EP yake katika vyombo husika. Huku akisisitiza Mashabiki kukaa mkao wa kuipokea Albam yake ya kwanza kwani yuko kwenye maandalizi ya kutayarisha Albam.