MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Liverpool, chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Jurgen Klopp. Mohamed Salah amecheka alipoulizwa kuhusu suala la kuwa nafasi ya sita kwenye tuzo za Ballon d’Or.
Kwenye tuzo nyota huyo alishika nafasi ya sita huku namba moja ikiwa mikononi mwa Lionel Messi anayekipiga ndani ya PSG.
Kutwaa tuzo hiyo Messi anakuwa ni namba moja kwa wachezaji waliochukua tuzo nyingi akiwa nazo saba kuanzia ameanza kucheza soka.
Juzi Salah alifanikiwa kufunga mabao mawili wakati timu ya Liverpool ilipocheza dhidi ya Everton na kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Goodison Park.
“Sina maneno yoyote ya kuhusu hilo, nawashukuru sana,” alisema Salah huku akicheka alipoulizwa kuhusu namna anavyojiskia kuwa nafasi ya sita.