MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Jesse Lingard mwenye miaka 28 anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho kwenye kipindi cha usajili wa Januari,mwakani.
Msimu uliopita nyota huyo alikuwa kwa mkopo ndani ya kikosi cha West Ham United na aliweza kufanya vizuri lakini aliporejea ndani ya Manchester United hana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo ameweka wazi kwamba anataka kuondoka kwenye kikosi hicho ili aweze kupata changamoto mpya pamoja na nafasi ya kucheza kwa muda mrefu.
Staa huyo atasepa mwakani bure kwa kuwa mkataba wake unameguka mwakani hivyo anakwenda kuanza maisha mapya kwa kuwa aligoma kufanya mazungumzo ya kuongeza dili jipya na anatajwa kuwa kwenye rada za Barcelona ya Hispania pamoja na AC Milan ya Italia.