BAADA ya dakika 90 kukamilika kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Ruvu Shooting v Simba uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting alikuwa kwenye jukumu zito la kutimiza majukumu ya taifa.
Ubao ulisoma Ruvu Shooting 1-3 Simba na kufanya mabingwa hao watetezi kusepa na pointi tatu jumlajumla.
Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere ambaye alitupia mabao mawili huku moja likifungwa na Kibu Dennisi ilikuwa ni ndani ya dakika ya dakika 45 Simba iliweza kuweza kushinda mabao hayo.
Kwa upande wa Ruvu Shooting alikuwa ni Elias Maguli ambaye alitibua hesabu za Aishi Manula kusepa na clean sheet ya sita kwa kuwa alimtungua dakika ya 70.
Bwire alipoulizwa na Waandishi wa Habari kuhusu mchezo huo alionekana akiwa kwenye majukumu mengine na kusema:”Nipo kwenye majukumu ya kitaifa kwa sasa, halo haloo afande chai, afande chai,”.
Ushindi wa Simba unaifanya ifikishe pointi 14 ikiwa nafasi ya pili huku Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 15 na Ruvu Shooting inabaki na pointi sita ikiwa nafasi ya 10.
Tayari kikosi cha Simba kimerejea Dar baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa jana Novemba 19.