Home Sports AZAM FC BILA DUBE MAJANGA

AZAM FC BILA DUBE MAJANGA

KWENYE safu ya ushambuliaji Azam FC kwa sasa inapata tabu kwelikweli bila ya uwepo wa Prince Dube ambaye anatibu majeraha yake kwa kuwa hakuna mchezaji ambaye ameweza kufikia rekodi ya mabao ambayo aliweza kufunga baada ya kucheza mechi tano.

Kwenye mechi tano msimu wake wa kwanza wa 2020/21 nyota huyo alifunga jumla ya mabao sita na alitoa pasi moja ya bao kwenye ligi.

Dube alianza kucheka na nyavu kwenye mchezo wa kwanza ambapo alianza kufunga bao moja mbele ya Polisi Tanzania,Septemba 7, Uwanja wa Azam Complex,alitupia mabao mawili mbele ya Coastal Union, Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex.

Septemba 26 alitupia mbele ya Polisi Tanzania bao moja na alifunga mabao mawili pamoja na pasi moja mbele ya Kagera Sugar ilikuwa Oktoba 4.

Kwa sasa washambuliaji wote wapya wa Azam FC ikiwa ni pamoja na Idris Mbombo na Rodgers Kola hakuna ambaye amefikia rekodi hii kwa kuwa kila mmoja ametupia bao moja na kwenye mechi tano Azam FC imefunga mabao manne.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ikiwa imecheza jumla ya mechi tano ndani ya dakika 450 imekusanya pointi 7 baada ya kushinda mechi mbili imepoteza mbili na kukusanya sare moja.

Dube aliweza kuwa namba moja kwa utupiaji katika kikosi cha Azam FC ambapo baada ya msimu kukamilika alitupia jumla ya mabao 14 na pasi tano za mabao.

Previous articleKMC V AZAM FC YAMEFUNGWA MABAO 13
Next articleLINGARD ANATAKA KUSEPA UNITED