Home Sports KMC V AZAM FC YAMEFUNGWA MABAO 13

KMC V AZAM FC YAMEFUNGWA MABAO 13

JUMLA ya mabao 13 yamefungwa kwenye mechi sita ambazo wamekutana wababe wawili KMC na Azam FC.

Klabu ya Azam FC wao wametupia mabao nane, huku KMC ikifunga mabao matano kwenye mechi za ligi.

Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zake za nyumbani ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC, Novemba 21, Jumapili.

Mchezo huounatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru ambapo timu zote zinapiga hesabu ya kusepa na pointi tatu muhimu.


Rekodi zinaonyesha kwamba Azam FC imeshinda nusu ya mechi hizo ikifanya hivyo mara tatu, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

 
 Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 9 na pointi 7 baada ya kucheza mechi tano huku KMC ikiwa nafasi ya 16 na pointi mbili baada ya kucheza pia mechi tano.
Kuelekea mchezo wa kesho Azam FC watakosa huduma ya nyota wao Prince Dube ambaye ni namba moja kwa utupiaji msimu wa 2020/21 alipotupia mabao 14 na pasi tano ila kuna ingizo jipya ikiwa ni pamoja na Mbombo Idris pamoja na Rodgers Kola kwenye safu ya ushambuliaji.
Previous articlePABLO AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA,CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleAZAM FC BILA DUBE MAJANGA