NYOTA HAWA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA POLISI TANZANIA
KUMEIBUKA taarifa kuwa Polisi Tanzania wapo kwenye mpango wa kuwasajili viungo wawili wa Azam FC, Mudathir Yahya na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ ambao wamesimamishwa. Taarifa hizo zinadai kuwa, Polisi Tanzania wanawataka nyota hao ili kuimarisha kikosi chao na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi mwisho wa msimu. Chanzo hicho kililiambia Spoti Xtra kuwa: “Upo mpango wa Azam FC kuachana na Mudathir pamoja na Sure…