BEKI MATATA AREJEA BARCELONA

DANI Alves beki matata mwenye mataji kibao ikiwa ni mafanikio yake makubwa kwa sasa amerejea tena ndani ya Barcelona baada ya kusepa hapo miaka mitano iliyopita ambapo aliibukia ndani ya Juventus na ikigota Januari anaanza kuvaa uzi wa Barcelona.

 

Ni makubaliano ya kikanuni ambayo Barcelona wamefikia kwa kuamua kumpa dili beki huyo wa makombe raia wa Brazil kwa lengo la kuongeza makali katika safu ya ulinzi.

Nyota huyo ni pendekezo namba moja la Kocha Mkuu wa Barcelona, Xavi Hernandez ambaye ametangazwa kuinoa timu hiyo baada ya kuchimbishwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ronaldo Koeman.

Barcelona wenyewe wamesema kuwa wamemrejesha nyumbani beki wa kazi ambapo rekodi zinaonyesha kuwa ametwaa mataji 46 ambapo akiwa na Barcelona alitwaa mataji 23,Juventus mawili, PSG mataji sita, Sao Paulo taji moja na akiwa na Sevilla mataji matano.