>

NABI ATAKA REKODI HII YANGA

KOCHA wa Yanga, Nasrredine Mohamed Nabi, amefunguka kuwa anahitaji timu yake iwe na uwezo mkubwa zaidi wa kumiliki mpira na kuwa na rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye kila mechi.

 

Nabi alisema soka la kisasa limebadilika sana kwa sababu timu yenye uwezo wa kumiliki mpira muda mrefu na kupiga pasi nyingi ndiyo huwa na nafasi ya kushinda mchezo kwa sababu wachezaji wanaongeza kujiamini.

 Nabi amesema timu yake imekuwa na uwiano mzuri kwenye kupiga pasi na kumiliki mpira, ila bado kuna kitu kidogo hakijakaa sawa na anakifanyia kazi baada ya muda mfupi timu hiyo itakuwa tishio zaidi kwenye pasi.


“Nahitaji timu 
yangu na wachezaji wawe na uwezo wa kumiliki mpira zaidi ya sasa. Ubora wa kupiga pasi uwe juu zaidi na tuwe kati ya timu ambazo zina idadi kubwa ya pasi.


“Timu inayofanya hivyo 
hujiweka kwenye mazingira mazuri ya kushinda mchezo. Kadiri unavyokaa na mpira muda mrefu timu inaongeza kujiamini na kumchanganya mpinzani, hicho ndiyo tunahitaji,” amesema Nabi.