KAMBI ya muda iliyowekwa na vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga inatajwa kuwaimarisha mastaa wa timu hiyo jambo ambalo limemfurahisha kocha wa timu hiyo Nasreddine Nabi.
Novemba 9, Yanga ilikuwa ndani ya Bahari ya Hindi na kuibukia Zanzibar ambapo ilikuwa na mechi mbili za kirafiki kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea mechinza ligi na ilishinda zote mbili.
Jana, Novemba 13 kikosi cha Yanga kilirejea salama Dar kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Novemba 20, Uwanja wa Ilulu,Lindi .
Mechi ya kwanza Novemba 9, Uwanja wa Amaan baada ya dakika 90 ulisoma Mlandege 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Heritier Makambo.
Mchezo wa pili ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma KMKM FC 1-2 Yanga ni mabao ya Fiston Mayele na Jesus Moloko na kukamilisha dakika 180 bila kupoteza.
Nabi amesema:”Wachezaji wapo viziri na wanajitahidi kutimiza majukumu yao, bado tunazidi kuimarika hivyo mashabiki wawe nasi bega kwa bega,”.
Miongoni mwa mastaa ambao walikuwa na Yanga Zanzibar ni pamoja na Deus Kaseke, Fiston Mayele,Abdalah Shaibu,’Ninja.