SABABU YA CHAMA KUKAA BENCHI YATAJWA

KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, amefunguka suala la kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama, kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho huku akiweka wazi kuwa mchezaji huyo anahitaji muda zaidi wa kukaa sawa ndani ya timu hiyo.


Chama alijiunga na RS Berkane 
mwanzo wa msimu huu akitokea Simba sambamba na winga wa zamani
wa Yanga, Tuisila Kisinda.


Ibenge amesema kuwa suala la Chama kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya timu hiyo inatokana na mchezaji huyo kushindwa kuendana haraka na mazingira ya timu
jambo ambalo linahitaji muda kidogo 
kwa mchezaji huyo kukaa sawa.


“Chama kushindwa kupata nafasi 
ya kucheza mara kwa mara inatokea kwa wachezaji wengi wakubwa
duniani ambao baada ya kuhama 
kutoka sehemu moja kwenda nyingine wanashindwa kuendana na mazingira
ya timu haraka jambo ambalo baadaye 
hubadilika baada ya kuyazoea mazingira, ni kama tu ilivyotokea kwa Chama.


“Hivyo Chama anahitaji muda wa 
kuyazoea mazingira ya timu ambayo ni mpya kwake, naamini atakuja
kukaa sawa, Chama ni mchezaji mzuri 
mwenye uwezo mkubwa wa kucheza timu yoyote barani Afrika, hivyo ndio
maana hata sisi tulimsajili, naamini 
kila kitu kitakuwa sawa huko mbeleni, ni jambo la muda tu,” alisema kocha
huyo.