MOHAMED Salah Mwafrika ambaye anawatesa Wazungu ndani ya Ligi Kuu England pamoja na mashindano mengine kwa sasa yeye ni wakucheka na minyavu tu ameongoza kilio leo kuelekea Manchester United.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao umechezwa leo Uwanja wa Old Trafford ubao umesoma Manchester United 0-5 Liverpool.
Mabao ya Naby Keita ambaye alifungua pazia dakika ya 5, Diogo Jota dakika ya 13, Salah kafunga hat trick ilikuwa ni dakika ya 38,45 na 50.
Majanga kwa Manchester United yaliiandama timu hiyo kwa kuwa staa wao Paul Pogba ameonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 60 na kuwafanya wamalize mchezo wakiwa pungufu.