BAADA ya kikosi cha Simba kufungashiwa virago leo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa Uwanja wa Mkapa kwa kufungwa mabao 3-1 Haji Manara alaiyekuwa Ofisa Habari wa timu hiyo ametupa dongo kimtindo.
Manara kwa sasa yupo zake ndani ya Yanga akiwa no Ofisa Habari wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia.
Muda mfupi baada ya Simba kupoteza na ubao kwenye mchezo huo kisha kuangukia katika Kombe la Shirikisho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika namna hii:-Alhamdulillah.
“Hamuwezi viongozi wenu kutuma ….. kunitusi kila siku na kunifanyia visa vya kila aina wakati niliwekeza nguvu na akili zangu hapo,kisha mbaki salama.
Mungu hulipa hapa hapa duniani na malipo mabaya zaidi yanakuja kwenu. Hiyo ni Trela Movie kamili inakuja,,msimu huu mtapoteza kila mlichoshinda,” .
Alisindikiza na picha ya matokeo ya leo Uwanja wa Mkapa kwenye ujumbe huo.
Bao pakee la Simba lilifungwa na Rally Bwalya dakika ya 41 kisha Jwaneng walijibu mapigo dakika ya 46 na 59 kupitia kwa Rudath Wendell na ule msumari wa maumivu ulipachikwa na Gape Mohutsiwa dakika ya 86.