>

AZAM FC SAFARI YAO KIMATAIFA YAKWAMIA MISRI

KUPOTEZA kwa Azam FC ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho usiku wa kuamkia leo na Pyramids kumewafungashia virago mazima.

Safari ya Azam FC kutinga katika hatua ya makundi imekwamia nchini Misri ambapo ndani ya dakika 45 za mwanzo wapinzani wao waliweza kumaliza mchezo kwa kupata bao pekee la ushindi.

Ubao wa June 30 nchini Misri baada ya dakika 90 ulisoma Pyramids 1-0 Azam FC jambo lililowaondosha wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Ni bao la Aly Gabr Mossad dakika ya 29 liliipa nguvu Pyramids ya Misri na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-0 Pyramids.

Azam FC sasa watarejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara ambapo wana kazi ya kusaka ushindi Oktoba 30 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.