STAA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ametembeza mkwara mzito kwa kubainisha kwamba atawafunga mdomo wale wanaoikosoa timu hiyo kwa sasa.
Ronaldo ambaye ni ingizo jipya ndani ya United ambapo aliibuka huko akitokea ndani ya kikosi cha Juventus amebainisha kwamba anachukia kuona timu hiyo inafeli.
Nyota huyo anaamini kwamba timu hiyo inapitia kipindi kigumu kwa muda lakini itakuwa salama na itapata matokeo katika mechi zijazo tofauti na wengi wanavyofikiria.
“Lengo langu kuja hapa ilikuwa ni kushinda na ninaamini kwamba itakuwa hivyo japo nimekuwa nikikosolewa pamoja na timu yangu mara kwa mara.
“Katika hilo ninajua kwamba nitawafunga mdomo kwenye hilo kwa kushinda ipo wazi na tutafanya vizuri kwa kuwa tupo imara na wachezaji wengine wapo tayari,”.
Leo United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 12:30 jioni Uwanja wa Old Trafford.