UWANJA wa Stamford Bridge leo Oktoba 23 umekusanya jumla ya mabao 7 ambayo yamefungwa na Chelsea wakiikandamiza Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Mason Mount alitupia hat trick yake kwa kupachika mabao dakika ya 8,85 kwa penalti na dakika ya 90 huku mengine yakipachikwa na Callum Hudson-Odoi dakika ya 18, Reece James dakika ya 42, Ben Chilwell dakika ya 57 na Max Aarons alijifunga dakika ya 62.
Pia B Gibson wa Norwich alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Ushindi huo unaifanya Chelsea kuwa na uhakika wa kukaa namba moja katika msimamo wa Ligi Kuu England kwa wiki nyingine tena licha ya kuwa na majeraha ya nyota wao wakubwa.
Chelsea haikuwa na Romelu Lukaku na Timo Werner wote walikosa mchezo jambo ambalo lilikuwa likimpasua kichwa Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ila ameona kazi ilifanywa na vijana wake.