Home Sports SIMBA WAPO TAYARI KIMATAIFA

SIMBA WAPO TAYARI KIMATAIFA

 

HITIMANA Thiery, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Jwaneng Galax ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo utakuwa ni wa marudio baada ya ule wa awali Simba kucheza ugenini nchini Botswana.

Ilikuwa ni Oktoba 17 ambapo Simba waliweza kushuka uwanjani katika kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na waliweza kusepa na ushindi.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Jwaneng Galaxy 0-2 Simba na John Bocco na Taddeo Lwanga hawa walipeleka msiba kwa Waswana hao ambao wana hasira ya kulipa kisasi kesho kwa Mkapa.

Hitimana amesema:”Wapinzani wetu wanahitaji kushinda kwenye mchezo wetu wa marudio ndio maana wamekuja hata sisi pia tunahitaji ushindi ndio maana tunajiandaa.

“Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wapo sawa kwa ajili ya mchezo wetu ujao hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwa bega kwa bega na sisi ili tuweze kusonga mbele,”.

Ikiwa Simba itashinda ama kupata sare itakuwa imefungua njia na kutinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ambayo ni kubwa na ya muhimu kwa Tanzania inayowakilishwa na Simba kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleKMC WAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA NAMUNGO,ILULU
Next articleCHELSEA WATEMBEZA 7 G HUKO BILA LUKAKU