OKTOBA 24 leo kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kinatarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utakuwa ni wa marudio.
Katika mchezo wa kwanza, Simba ilishinda mabao 2-0 hivyo leo ina kazi ya kulinda ushindi wake pamoja na kusaka ushindi ili kuongeza nafasi ya kutinga hatua ya makundi.
Hiki hapa kikosi ambacho kinatarajiwa kuanza ni kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra Jumapili ambalo lipo mtaani leo kwa 500 tu:-
Aishi Manula
Pascal Wawa
Shomari Kapombe
Henock
Mohamed Hussein
Hassan Dilunga
Taddeo Lwanga
Rally Bwalya
Sadio Kanoute
John Bocco
Bernard Morrison