
MIANZINI MABINGWA WA MERIDIAN BET STREET SOCCER BONANZA
KLABU ya Mianzini FC kutoka Temeke Jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuibuka Mabingwa wa Meridian Bet Street Soccer Bonanza yaliyofanyika Desemba 18 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwembeyanga. Mianzini walitwaa ubingwa huo baada ya kuwachapa TP City FC kwa mikwaju 4-3 ya Penalti baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 0-0…