
SURE BOY APEWA MIAKA MIWILI YANGA
RASMI kiungo mchezeshaji wa Azam FC, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu usajili wa dirisha dogo ufunguliwe Desemba 16, mwaka huu. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga baada ya hivi karibuni kumsaini kiungo mshambuliaji wa Biashara United, Denis Nkane. Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Spoti Xtra, kiungo huyo alisaini mkataba huo baada ya kuvunja mkataba wake na Azam FC. Mtoa taarifa…