
BODABODA 8 KUWA MIKONONI MWA WATANZANIA KUTOKA HALOPESA
KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania ya Halotel Tanzania,leo Machi 28 imezindua promosheni ya ‘Shinda na Halopesa’ itakayotoa fursa kwa wateja kuweza kushinda fedha taslimu pamoja na Pikipiki maarufu kama ‘Bodaboda’ mpya kabisa. Promosheni hii itadumu kwa muda wa wiki 8 ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa na ni jumla ya wateja 72 watashinda zawadi mbalimbali zitakazotolewa…