KOCHA NABI APIGA MKWARA KUHUSU UBINGWA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo, kwa kuwaambia waache presha anajua jambo la kufanya ili kuweza kutwaa ubingwa wa ligi. Kauli hiyo ameitoa mara baada ya wapinzani wao Simba walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 kupata matumaini ya kutetea ubingwa kufuatia Yanga kupata suluhu tatu mfululizo….

Read More

PABLO ATUMA UJUMBE HUU KWA PAMBA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Pamba. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku na mshindi wa mchezo anakwenda kukutana na Yanga hatua ya nusu fainali. Pablo amesema kuwa kuna ushindani mkubwa ambao upo kwenye Kombe…

Read More

KIUNGO WA KAZI APEWA MWAKA MMOJA YANGA

KIUNGO mshambuliaji mkongwe Mrundi, Said Ntibanzokiza ‘Saido’, amepewa mkataba wa mwaka mmoja wenye masharti magumu katika Klabu ya Yanga. Mrundi huyo ambaye anasubiria utambulisho hivi sasa, hivi karibuni aliongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo utakaomalizika 2023. Saido ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu akiwa…

Read More

DODOMA V YANGA KUPIGWA SAA 10:00 JIONI

MECHI ya Yanga dhidi ya Dodoma Jiji ambayo inatarajiwa kuchezwa Jumapili, Uwanja wa Jamhuri imebadilishwa muda kutoka ule uliopangwa awali. Awali ilikuwa ni saa 1:00 usiku mchezo huo wa ligi uchezwe na sasa unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni. Sababu za mchezo huo kubadilishwa muda ni kutokana na uwanja huo kuwa na matumizi mengine. Tayari timu…

Read More

NAMUNGO V MBEYA KWANZA MCHEZO HAUJACHEZWA,TIMU ZIMESEPA

MCHEZO kati ya Namungo FC dhidi ya Mbeya Kwanza ambao ulitarajiwa kuchezwa leo Mei 13 umeweza kusimamishwa na haujachezwa kutokana na kutokuwepo kwa gari ya wagonjwa. Kabla ya mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu,hakukuwepo na gari ya kubebea wagonjwa, (Ambulance). Hata hivyo muda ambao waliweza kukaa kwa kusubiri gari la wagonjwa kwa muda wa…

Read More

BREAKING:MORRISON ASIMAMISHWA SIMBA

TAARIFA rasmi kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa mchezaji wao Bernard Morrison amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba umeeleza kuwa umempa mapumziko ya muda mpaka mwisho wa msimu mchezaji huyo. Taarifa imeeleza kuwa wamefikia hapo ili kumpa muda wa Morrison kushughulikia mambo yake…

Read More

KAGERA SUGAR KUKOMAA MECHI ZIJAZO

FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa watajipanga kwa ajili ya mechi zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara. Mchezo uliopita Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba na kuweza kuyeyusha pointi tatu mazima. Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa wamekuwa kwenye ratiba ngumu jambo ambalo linawafanya washindwe kwenda na…

Read More

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MORRISON

UONGOZI wa Simba umesema kuwa ikiwa watapata taarifa kwamba mchezaji wao Bernard Morrison anahitajika na Yanga watawapa hata kwa mkopo. Nyota huyo ambaye kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa muda kwa kile ambacho Kocha Mkuu, Pablo Franco wa Simba amesema kwamba ana majeraha amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga. Ikumbukwe kwamba Yanga ilikuwa ni timu ya mwanzo…

Read More

KICHUYA AINGIA ANGA ZA SIMBA

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wanafikiria namna ya kuweza kumrudisha nyota wao wa zamani ndani ya kikosi hicho Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo FC. Kichuya aliwahi kucheza Simba ambapo alijiunga na timu hiyo Julai 2016 kisha akasepa 2019 kuelekea Misri na akarudi tena ndani ya Simba Januari 15,2020 mwanzoni mwa msimu wa 2020/21…

Read More

KANE ALIKUWA MWIBA MBELE YA ARSENAL

STAA wa Tottenham Harry Kane alikuwa ni mwiba mkali mbele ya Arsenal baada ya kuwatungua mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Alianza kufunga dk ya 22 kwa mkwaju wa penalti kisha bao la pili alipachika dk ya 37 na msumari wa tatu ulipachikwa na nyota Son ilikuwa dk ya 47. Mpaka dk 90…

Read More

KMC:TUPO KWENYE NAFASI MBAYA

KOCHA Mkuu wa KMC, Hitimana Thiery amesema kuwa wanachoangalia kwa sasa ni mechi zote zilizobaki kupata ushindi kwa kuwa wapo kwenye nafasi mbaya. Akizungumza na Saleh Jembe,amesema kuwa pointi 27 walizonazo sio salama licha ya kushinda mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar. “Tulianza kucheza vizuri mwanzo na tukapata nafasi kwa kumiliki na wapinzani wetu waliweza…

Read More

YANGA YAGOMEA SARE TENA KWENYE LIGI

MARA baada ya kupata suluhu katika michezo mitatu mfululizo kwenye ligi kuu, benchi la ufundi la timu hiyo, limesema kuwa kwa sasa inatosha na litapambana kuhakikisha kuwa timu hiyo inapata ushindi katika michezo inayofuata na kuendeleza matumaini ya ubingwa msimu huu. Yanga imeshindwa kupata ushindi wala kufunga bao katika michezo mitatu iliyopita mfululizo dhidi ya…

Read More

SIMBA:TUNALITAKA KOMBE LETU

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba unahitaji kuteteta taji la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwao hivyo watapambana kupata matokeo. Kesho, Mei 14 Simba ina kazi ya kusaka ushindi mbee ya Pamba katika mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Ahmed Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani…

Read More