Home Sports NAMUNGO V MBEYA KWANZA MCHEZO HAUJACHEZWA,TIMU ZIMESEPA

NAMUNGO V MBEYA KWANZA MCHEZO HAUJACHEZWA,TIMU ZIMESEPA

MCHEZO kati ya Namungo FC dhidi ya Mbeya Kwanza ambao ulitarajiwa kuchezwa leo Mei 13 umeweza kusimamishwa na haujachezwa kutokana na kutokuwepo kwa gari ya wagonjwa.

Kabla ya mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu,hakukuwepo na gari ya kubebea wagonjwa, (Ambulance).

Hata hivyo muda ambao waliweza kukaa kwa kusubiri gari la wagonjwa kwa muda wa dk 15 hakukuwa na gari la wagonjwa.

Pia mpaka dk ya 20 inafika hakukuwa na gari la wagonjwa ambapo inaelezwa kuwa gari lilikuwepo lakini liliweza kuondoka kwa kupata dharula.

Na kumekuwa na mvutano kati ya wasimamizi wa mechi na Mbeya Kwanza ambapo wanasema kuwa hawakuliona gari la wagonjwa.

Baada ya gari la waamuzi kuweza kufika saa 10:24 Mbeya Kwanza hawakuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo wakaamua kuondoka na Namungo nao waliweza kuendelea kukaa hapo kwa muda kisha wakaondoka.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni maamuzi ya kamati ili kuweza kujua hatma ya mchezo wa leo.

Previous articleBREAKING:MORRISON ASIMAMISHWA SIMBA
Next articleUKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI