Home Sports KMC:TUPO KWENYE NAFASI MBAYA

KMC:TUPO KWENYE NAFASI MBAYA

KOCHA Mkuu wa KMC, Hitimana Thiery amesema kuwa wanachoangalia kwa sasa ni mechi zote zilizobaki kupata ushindi kwa kuwa wapo kwenye nafasi mbaya.

Akizungumza na Saleh Jembe,amesema kuwa pointi 27 walizonazo sio salama licha ya kushinda mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Tulianza kucheza vizuri mwanzo na tukapata nafasi kwa kumiliki na wapinzani wetu waliweza kupata nafasi mbili ambazo walizitumia kwenye mchezo wetu.

“Kwa Sasa ni kuangalia timu isiweze kushuka na unaona kwamba tunapishana kwa pointi chache sana na wale wa chini ni pointi ya mechi moja hapo ni lazima tuangalie namna gani tutaweza kusogea mbele ya hapa tulipo.

“Kwenye mechi sita hatukuwa na matokeo na ligi ni ngumu na malengo yetu ni kuona hatuwezi kuwa hapa tulipo tunataka kusogea mbele,”

KMC ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ni jana iliweza kushinda baada ya kutoka kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-1.

Previous articleYANGA YAGOMEA SARE TENA KWENYE LIGI
Next articleKANE ALIKUWA MWIBA MBELE YA ARSENAL