Home Sports KAGERA SUGAR KUKOMAA MECHI ZIJAZO

KAGERA SUGAR KUKOMAA MECHI ZIJAZO

FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa watajipanga kwa ajili ya mechi zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mchezo uliopita Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba na kuweza kuyeyusha pointi tatu mazima.

Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa wamekuwa kwenye ratiba ngumu jambo ambalo linawafanya washindwe kwenda na kasi ya ushindani.

“Kuna mechi nyingi tumecheza hivi karibuni lakini haina maana kwamba hatuna uwezo wa kucheza mechi nyingine lazima tupambane ili kuwa imara.

“Ngumu kuona kwamba tunafurahi kupata matokeo mabaya lakini ambacho tunahitaji ni kuwa imara na kusonga mbele zaidi kwenye mechi zijazo za ligi,” amesema.

Previous articleSIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MORRISON
Next articleBREAKING:MORRISON ASIMAMISHWA SIMBA