
ALIOU CISSE,KOCHA BORA CAF
ALIOU Cisse, amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Aliou Cisse, 46, aliiongoza Senegal kushinda kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon, mapema mwaka huu, baada ya kuishinda Misri kwa mikwaju ya penalti. Pia ameiongoza Simba wa Teranga kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka huu…