Home Sports KIUNGO WA MALI KUONDOKA SIMBA

KIUNGO WA MALI KUONDOKA SIMBA

MZEE wa mikato ya kimyakimya,kiungo mgumu ndani ya Simba, Sadio Kanoute huenda akauzwa ili apate changamoto mpya.

Inaelezwa kuwa kiungo huyo amepata dili kutoka kwa timu za nje ambazo zinahitaji saini yake ikiwa ni pamoja na zile za nyumbani kwao Mali pamoja na Afrika Kusini.

Kaizer Chiefs inatajwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini ya kiungo huyo.

Mbali na kupata ofa pia anatajwa kujadiliwa na mabosi wa Simba ambao wanahitaji kumuuza ili aweze kutoa nafasi ya kusajili nyota mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Simba wanafikiria wachezaji wa kimataifa wa kuweza kuachana nao ili waweze kukidhi idadi ya wachezaji 12 wanaotakiwa na Shirikishisho la Soka la Tanzania,(TFF).

Previous articleAZAM FC KAMBI IMEPAMBA MOTO,KESHO KUSEPA
Next articleBAADA YA KUFUNGIWA MANARA AFUNGUKA