Mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu kama Depú, amewekwa sokoni na klabu yake ya Yanga SC baada ya kuwasili kwa washambuliaji wawili wapya wa kigeni katika kikosi hicho.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya mabingwa hao wa Tanzania kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji, hivyo kuona ni vyema kumpa nafasi Depú kutafuta changamoto mpya.
Kwa upande mwingine, klabu yake ya zamani ya Petro de Luanda imeonyesha nia ya kumrejesha mshambuliaji huyo Angola, lakini mazungumzo kati ya pande hizo bado hayajafikia makubaliano.