
JUKUMU LA PETER BANDA HILI HAPA
SIMBA imeweka wazi kuwa mara baada ya kiungo mshambuliaji wao, Peter Banda kurejea nchini akitokea Cameroon alipokuwa na kibarua cha kuiwakilisha Malawi kwenye mashindano ya Afcon, moja kwa moja atajiunga na programu za maandalizi ya michezo ijayo hususani mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imepangwa kwenye Kundi D pamoja na timu za…