Home Sports SIMBA KAZINI UWANJA WA MAJALIWA

SIMBA KAZINI UWANJA WA MAJALIWA

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuwa uwanjani leo kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Namungo, Aprili 30 2024.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma Simba 1-1 Namungo FC walipogawana pointi mojamoja.

Mchezo uliopita kwa Simba ambao ulikuwa ni wa mwisho kwa Abdelhakh Benchikha kukaa benchi ilikuwa Aprili 20 2024 alishuhudia ubao ukisoma Yanga 2-1 Simba.

Leo kikosi cha Simba kipo mikononi mwa Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola.

Kuna nyota ambao watakosekana ambao ni Clatous Chama, Luis Miqussone, Shomari Kapombe kwa kuwa bado hawajawa fiti.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amebainisha kwamba wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu tupo tayari na mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwa pamoja nasi,”.

Previous articleMTIBWA SUGAR KWENYE NYAKATI NZITO
Next articleUWANJA WA MAJALIWA NAMUNGO WAGAWANA POINTI NA SIMBA