Home Sports MASHUJAA SIO KINYONGE WATUMA UJUMBE SIMBA

MASHUJAA SIO KINYONGE WATUMA UJUMBE SIMBA

WAPINZANI wa Simba kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Lake Tanganyika, Mashujaa wamegomea unyonge mbele ya Mnyama kwa kubainisha kwamba wamefanya maandalizi mazuri kuwakabili.

Ipo wazi kwamba baada ya kumaliza ngwe ya kimataifa Simba ikigotea hatua ya robo fainali ina kazi kwenye mashindano ya ndani ambayo ni Ligi Kuu Bara pamoja na CRDB Federation Cup.

Aprili 9 watakuwa wageni mbele ya Mashujaa mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Kocha Mkuu wa Mashujaa, Mohamed Abdallah,(Bares) ameweka wazi kuwa anatambua mpinzani wake namna alivyo imara kutokana na kushiriki mashindano ya kimataifa lakini wamejiandaa vizuri.

“Simba wameonyesha kiwango kizuri kimataifa hilo tunalitambua licha ya kwamba wameondolewa katika mashindano hayo. Sisi tumejipanga kwa hilo katika mashindano haya”.

“Tumekuwa na muda mzuri wa maandalizi na sasa tunakwenda kufanya kazi yetu uwanjani licha ya kwamba hali ya hewa imekuwa ngumu kuturuhusu kufanya mazoezi kwa asilimia kubwa uwanjani, tupo tayari,”.

Previous articleKARIAKOO DABI HII HAPA KITAWAKA
Next articleKUTANA NA SLOTI YA BURSTING HOT 5 KASINO YA MERIDIANBET