Home Sports KARIAKOO DABI HII HAPA KITAWAKA

KARIAKOO DABI HII HAPA KITAWAKA

ZINAHESABIWA siku kwa sasa kutokana na tarehe kuwa wazi kwa kuwa tayari imeshapangwa na taarifa kwa kila timu zimefika mahali pake kwa mujibu wa taarifa.

Ikumbukwe kwamba Yanga na Simba walikuwa na kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wamegotea wote hatua ya robo fainali.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza tarehe ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba “Kariakoo Derby’ ambayo itakuwa ni Aprili 20 2024 Uwanja wa Mkapa.

Muda wa Kariakoo dabi itakuwa ni saa 11:00 jioni kwa kila timu kuwa uwanjani kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TPLB, Aprili 7 imeeleza namna hii “Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeupangia tarehe mchezo namba 180 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2023\24 kati ya Yanga na Simba maarufu kama ‘Kariakoo Derby’.

“Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba ilioyofanyiwa marekebisho na kutangazwa Februari 2024, sasa utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 20, 2024 saa 11:00 jioni.

“Klabu za Yanga na Simba na wadau wengine wa Ligi Kuu wamepatiwa taarifa zote kuhusu mchezo huo na maandalzi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mkubwa ya ligi sita kwa ubora barani Afrika,” taarifa imesema na kuongeza.

“Bodi ya Ligi inawatakia maandalizi mema ya wadau wote wa mchezo,”.

Novemba 5 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa kwenye mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba 1-5 Yanga. Pointi tatu mazima zilikwenda Jwangwani.

Previous articleSIMBA MIKONONI MWA MASHUJAA KIGOMA
Next articleMASHUJAA SIO KINYONGE WATUMA UJUMBE SIMBA