Home Sports SIMBA MIKONONI MWA MASHUJAA KIGOMA

SIMBA MIKONONI MWA MASHUJAA KIGOMA

BAADA ya kufungashiwa virago kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imerejea Bongo na ina kazi yakufanya kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC ya kutoka Kigoma.

Hivyo Simba ipo mikononi mwa Mashujaa kwenye msako wa ushindi ndani ya dakika 90 Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ipo wazi kwamba Simba imegotea hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukwama kutegua mitego yote kwa mara nyingine tena.

Katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0- 1 Al Ahly na ule mchezo wa mkondo wa pili nchini Misri ubao ulisoma Al Ahly 2-0 Simba ndani ya dakika 180 Simba imetunguliwa mabao matatu huku wakikwama kufunga mbele ya wapinzani wao.

Ni wazi kwamba Al Ahly ni mabingwa watetezi hivyo walikuwa wakicheza kibingwa kwenye mechi zote mbili nje ndani.

Kikosi hicho leo kimekwea pipa kuelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne CRDB Federation Cup.

Ni Aprili 9 mchezo huo unatarajiwa kwa kila timu zinapambana kusaka hatua ya kusonga mbele kwa kuwa timu itakayofungwa safari inamkuta mazima.

Previous articleVIDEO: YANGA WATOA TAMKO ZITO ISHU YA BAO LA AZIZ KI/MAKOMBE YANAFUATA
Next articleKARIAKOO DABI HII HAPA KITAWAKA