Home International RONALDO AZUA JAMBO, ASISITIZA KUNA MUUNGANIKO

RONALDO AZUA JAMBO, ASISITIZA KUNA MUUNGANIKO

CRISTIANO Ronaldo nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno amesisitiza kwamba timu hiyo ina muunganiko mkubwa huku kukiwa na nguvu kutoka nje zinazotaka kukivunja kikosi hicho.

Nyota huyo ameweka wazi kuwa nguvu hizo hazitaweza huku ikitajwa kwamba nyota huyo yupo tayari kusepa kabla ya mashindano ya Kombe la Dunia, Qatar,2022.

Ronaldo mwenye miaka 37 alijiunga na timu ya Taifa Ureno Qatar ikiwa ni muda mfupi kutoka kuachana na mabosi wake Manchester United ambao  walifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili, kwa sasa umaarufu wake unatajwa kuporomoka kutokana na matukio yake.

Ameandika rekodi yake ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao kwenye mashindano matano tofauti ya Kombe la Dunia ni baada ya kuwatungua Ghana ya Afrika kwa mkwaju wa penalti katika mchezo wao wa makundi ambapo alifunga bao hilo dakika ya 64 Ureno iliposhinda mabao 3-2 Ghana.

Ikumbukwe kwamba FIFA walimpoka bao alilodai amefunga kwenye mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Uruguay na aliyepewa bao hilo ni mpiga krosi, Bruno Fernandes, kutokana na hilo CR 7 alidai kuwa lile ni bao lake na anapaswa kupewa pia alipofanyiwa mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Korea Kusini alionekana kukasirika jambo ambalo lilileta kutolelewana kati yake na Kocha Mkuu.

Ronaldo hakuanza kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Uswisi na aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi jambo hilo pia halikumpa furaha kwa kuwa wakati wenzanke wakishangilia na mashabiki wao waliofunga safari ndefu mpaka Qatar yeye aliondoka uwanjani akiwa ameinamisha kichwa na kuwaacha wachezaji wenzake wakishingilia ushindi wa mabao 6-1.

 Mbadala wake kwenye mchezo huo mwenye miaka 21, Goncalo Ramos amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick kwenye mashindano ya Kombe la Dunia hatua ya 16 bora mwaka huu 2022 na mchezaji wa kwanza kufanya hivyo ilikuwa kwenye hatua ya mtoano mwaka 1990.

Kwa sasa nyota huyo wa zamani wa Manchester United hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Morocco na anatajwa kuwa aligomea mazoezi kwenye timu ya pili na wachezaji wenzake wa timu ya Ureno.

Gazeti la Ureno  linaloitwa Record limeeleza kuwa hiyo ilikuwa ni kero tangu awali ambapo Ronaldo alikuwa tayari kuachana na ndoto zake za Kombe la Dunia lakini chama cha Soka la Ureno kilimgomea mwamba huyo.

Taarifa zimeeleza kuwa Cristiano Ronaldo alikuwa tayari kuachana na timu hiyo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na kocha wa timu hiyo Fernando Santos.

Previous articleNI ZIPI ODDS KUBWA ZA MERIDIANBET MECHI ZA ROBO FAINALI WC 2022?
Next articleAZAM FC KUTUPA KETE YAO DHIDI YA MALIMAO