Home Sports AZAM FC YAKATA TAMAA ISHU YA UBINGWA

AZAM FC YAKATA TAMAA ISHU YA UBINGWA

KAIMU Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala amesema kuwa kushindwa kupata matokeo chanya kwenye mechi tatu kunawaondoa kwenye mbio za ubingwa.

Matajiri hao wa Dar mzunguko wa pili umekuwa ni mgumu kwao kupata matokeo ambapo walianza kupata sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Kagera Sugar na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold kisha ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Azam FC 2-3 Yanga.

Ongala amesema kuwa walikuwa kwenye umiliki mzuri wa mpira dhidi ya Yanga lakini walipoteza mchezo kwa makosa ambayo walifanya.

“Naona kwa sasa kwenye mbio za ubingwa hatupo kutokana na matokeo ambayo tumeyapata kwenye mechi za hivi karibuni lakini tutapambana kupata matokeo kwenye mechi zijazo.

“Tulicheza vizuri na tulipoanza kupata bao la kuongoza hilo lilifanya wachezaji kukwama kuongeza umakini na kufanya makosa ambayo wapinzani wetu waliyatumia,” .

Kwenye msimamo Aza, FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 18.

Mchezo ujoa wa Azam FC ni dhidi ya Mbeya City unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Desemba 31.

Previous articleMILIONI 30 MEZANI MNYAMA ATUNGULIWE KWA MKAPA
Next article10BET YAGAWA ZAWADI KWA WASHINDI PROMOSHENI KOMBE LA DUNIA