MILIONI 30 MEZANI MNYAMA ATUNGULIWE KWA MKAPA

    KLABU ya Tanzania Prisons imewekewa kitita cha Tsh Milioni 30 na wadhamini wao Kampuni ya Silent Ocean endapo itaifunga Simba.

    Prisons inatarajiwa kumenyana na Simba leo Desemba 30,2022 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa funga mwaka.

    Ikitokea wakashindwa kusepa na ushindi na kuambulia pointi moja watasepa na Milioni 10 kibindoni.

    Ikumbukwe kwamba hata mchezo waliocheza na Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa liliwekwa dauo nono kwa Prisons.

    Katika mchezo huo Prisons walicheza kwa kutumia nguvu kubwa huku safu ya ushambuliaji ikikosa umakini kwenye kumalizia nafasi wanazotengeneza.

    Ni jioni dakika ya 89 walitunguliwa bao moja na kiungo Feisal Salum na kuyeyusha fuko la hela walizowekewa mezani jumlajumla.

    Kazi nyingine ni leo mbele ya Simba ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Simba ilishinda bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Jonas Mkude.

    Previous articleVITA YA MATAJIRI, KAMA NOMA NA IWE, FEI AWACHENGA YANGA SC AIBUKIA JESHINI
    Next articleAZAM FC YAKATA TAMAA ISHU YA UBINGWA