Home Sports MABINGWA WATETEZI KUTUPA KETE YAO KWA MKAPA

MABINGWA WATETEZI KUTUPA KETE YAO KWA MKAPA

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Desemba 11 kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa raundi ya Pili Kombe la Shirikisho dhidi ya Kurugenzi.

Nabi hatakuwa kwenye benchi kwa kuwa anatumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu hivyo ni Cedric Kaze ambaye ni kocha msaidizi atakaa kwenye benchi.

Tayari vigogo wawili ambao ni Azam FC wao wametinga raundi ya 32 kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Malimao kwenye mchezo uliochezwa Desemba 9,2022 Uwanja wa Azam Complex.

Ni Simba nao Desemba 10 waliibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Eagle kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwa vigogo hawa kinara wa utupiaji ni Moses Phiri ambaye alitupia kambani mabao manne anafuatiwa na Mr Hat Tric, Abdul Seleman, ‘Sopu’ wa Azam FC na Clatous Chama wa Simba wenye mabao mawili.

Kaze ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini wamejiandaa kupata matokeo chanya.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu, tumejiandaa kupata matokeo na inawezekana kwa kuwa wachezaji wapo tayari,”.

Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa taji la Azam Sports Federation hivyo wakienguliwa safari ya utetezi itakuwa imegota mwisho.

Previous articleHAYA HAPA MAMBO YALIYOMUONDOA CEO BARBARA
Next articleSIMBA MATUMAINI MAKUBWA KUFANYA VIZURI