JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema ushindi wao mbele ya Eagle unawapa nguvu ya kuzidi kuimarika kwa mechi zijazo.
Ikiwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 10, ubao ulisoma Simba 8-0 Eagle na timu hiyo ikatinga hatua ya 32 Kombe la Shirikisho.
“Tumekuwa na mwanzo mzuri na hii inatupa nguvu kwa ajili ya mechi zijazo kufanya vizuri na inawezekana kutokana na namna wachezaji ambavyo wanajituma.