Home Sports YANGA YACHAPA MTU BAO 8-0 KWA MKAPA

YANGA YACHAPA MTU BAO 8-0 KWA MKAPA

KAMPENI ya kutetea ubingwa wa Kombe la Azam Sports Federation umeanza kwa ushindi mbele ya Kurugenzi.

Ni Yanga ambao ni watetezi wameibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Shukrani kwa Clement Mzize ambaye amefung bao la mapema ndani ya Kombe la Shirikisho dakika ya kwanza na aliibuka nyota wa mchezo kwa kuwa alipachika mabao manne.

Mabao mengine alifunga dakika ya 8,41 na msumari wa mwisho alipachika dakika ya 45 na kumfanya apige hat trick na kusepa na mpira wake.

Bao moja dakika ya 5 Kurugenzi kutoka Simiyu walijifunga kwenye harakati za kuokoa ilikuwa ni kupitia staa wao John.

Mabao mengine ya Yanga ambayo haikuwa na Fiston Mayele, Feisal yamefungwa na David Bryson dakika ya 75 huku Yusuph Athuman akitupia kambani mara mbili dakika ya 75 na 77.

Kurugenzi FC kipindi cha kwanza walikwama kuonyesha makeke yao mpaka kipindi cha pili angalau timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ilionyesha makeke yake.

Previous articleSIMBA MATUMAINI MAKUBWA KUFANYA VIZURI
Next articleBOSI YANGA:TUNAMTAKA YEYOTE, PHIRI ATOA UJUMBE MZITO