
AZAM YAMTANGAZA MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA COLOMBIA
Azam FC imetangaza mshambuliaji mpya kutoka Colombia, Franklin Navarro (24) ambaye amejiunga na timu yake hiyo mpya akitokea Cortuluá FC ya nchini kwao. Navarro anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam FC katika dirisha hili dogo la usajili.