
SIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA
MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kasi ya wapinzani wao Yanga huku akiahidi kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimbazi. Kauli hiyo ameitoa baada ya kuiona Yanga ikiwa kileleni ikiwa na pointi tisa, ikishinda michezo yakemitatu ya ligi katika msimu huu. Simba yenyewe imecheza michezo miwili kati ya hiyo wametoka suluhu na Biashara United huku ikiwafungaDodoma Jiji bao 1-0, lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere. “Mechi…