Home Sports MANARA:TUNA WAHESHIMU SIMBA,ILA TUNATAKA POINTI TATU

MANARA:TUNA WAHESHIMU SIMBA,ILA TUNATAKA POINTI TATU

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamewazidi wapinzani wao Simba pointi 13 ambazo ni nyingi.

Manara amesema kuwa hilo haliwafanyi waamini kwamba watashinda mchezo wao badala yake wanawaheshimu Simba.

“Tumewazidi pointi 13 na tunajua kwamba tuna uwiano mzuri kwa mabao ya kufungwa na kufungwa lakini haina maana kwamba tutawadharau wapinzani wetu hapa.

“Ambacho tunahitaji kwenye mchezo wetu huo ni pointi tatu na kila kitu kinakwenda sawa kwani ili uwe bingwa lazima ushinde mechi kubwa na ngumu,”

Aprili 30,2022 unatarajiwa kuchezwa mchezo kati ya Yanga v Simba,Uwanja wa Mkapa.

Previous articleSIMBA KUTUA BONGO LEO WAKITOKEA AFRIKA KUSINI
Next articleNAMNA REKODI DUME ILIVYOTIBULIWA UWANJA WA MKAPA