NAMNA REKODI DUME ILIVYOTIBULIWA UWANJA WA MKAPA

  ZILE ngome za ubishi kati ya vinara wa Ligi Kuu Bara,Yanga dhidi ya wakali kutoka kusini Namungo zimevunjwavunjwa na hatimaye mbabe ameweza kupatikana kwenye mchezo wa sita.

  Dakika 450 za machozi na jasho zimevunjwa

  Yanga imeibuka na ushindi baada ya kuweza kucheza mechi tano ambazo ni dk 450 bila kuambulia ushindi na badala yake wote walikuwa wanagawana pointi mojamoja.

  Kwenye dk hizo 450 za machozi na jasho yalikuwa yamepatikana mabao 10 na ni penalti moja iliweza kufungwa na Yanga kupitia kwa Said Ntibanzokiza huku waliyopata Namungo kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Bigirimana Blaise aliweza kukoa penalti hiyo.

  Ilikuwa ni msimu wa 2020 ambapo Bakari Mwamnyeto aliweza kumchezea faulo Shiza Kichuya ndan ya 18 na mwamuzi aliamuru ipigwe penalti huku Mwamnyeto akionyeshwa kadi ya njano.

  Kichuya wamoto 

  Shiza Kichuya kila wanapokutana na Yanga anakuwa kwenye ubora uleule huku mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto.

  Kwenye mchezo wa msimu wa 2020 alisababisha penalti na kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu wa 2021/22 alikuwa akiwasumbua mabeki wa Yanga na aliweza kufanya majaribio kutaka kumtungua Diarra Djigui.

  Mchezo wa juzi alifunga bao bora akiwa nje ya 18 na kuweza kuwa mmoja ya nyota waliomtungua Diarra kwa msimu huu kwenye ligi.

  Mayele kashindikana

  Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga ameshindikana kuzuilika kwa kuwa ameweza kutimiza ahadi yake aliyosema kwamba atawafunga Namungo wakikutana na kweli kawafunga.

  Awali aliwahi kusema atawafunga Azam FC na walipokutana Uwanja wa Azam Complex aliwatungua na sasa ana mabao 12 akiwa na pasi tatu za mabao ni kinara wa mabao ndani ya ligi.

  Namungo walijiamini kweli

  Namungo FC walicheza kwa kujiamini mbele ya Yanga na kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata jamo ambalo liliweza kuwagharimu na kupoteza mchezo huo.

  Kipindi cha kwanza safu ya ulinzi ilifanya makossa ambayo yaliipa nafasi Yanga kufunga kwenye mchezo huo na walipoweza kuongeza nafasi kipindi cha pili waliweza kuimarisha ngome yao na hawakufungwa.

  Feisal na Aucho wamerudi

  Alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha na walikosa mchezo dhidi Azam FC ila wapopewa nafasi mbele ya Namungo walifanya kwelie.

  Eneo la kati lilikuwa mikononi mwao na walikuwa kwenye kasi mwanzo mwisho katika mchezo huo walivuja jasho.

  Feisal alipachika bao la ushindi kwa Yanga na kuwafanya wavunje ule mwiko wa kutoifunga Namungo na wapo kileleni na pointi 54.

  Jamhuri Khiwelo, Kocha Msaidizi wa Namungo FC alisema kuwa rekodi ya kutofungwa imevunjwa na walikuwa wakihitaji kulinda rekodi ila ilishindikana.

  “Unajua yale yalikuwa maneno mwanzo kwamba tutashinda na hatuna hofu na Fiston Mayele, sasa unadhani nisingefanya hivyo ulitaka tufungwe mabao mengi? Hakuna ni matokeo uwanjani makosa tumefanya na tumepoteza,”.

  Cedrick Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga alisema furaha yao ni kupata pointi tatu kwenye mchezo mgumu dhidi ya Namungo FC.

  Previous articleMANARA:TUNA WAHESHIMU SIMBA,ILA TUNATAKA POINTI TATU
  Next articleSIMBA NDANI YA DAR,KANOUTE,INONGA,MANULA NDANI