Home Sports VAR YAMPA MAKASIRIKO PABLO FRANCO

VAR YAMPA MAKASIRIKO PABLO FRANCO

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hajui jambo gani ambalo lilitokea kwenye matumizi ya VAR hivyo hapendi kuzungumzia jambo hilo.

Simba ilikuwa inawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa imetolewa kwa kufungwa penalti 4-3 dhidi ya Orlando Pirates baada ya kuwa na jumla ya kufungana bao 1-1.

Walianza Simba kushinda mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa Dar walipokwenda Afrika Kusini walifungwa bao 1-0 na Orlando Pirates.

Pablo amesema hawezi kuzungumzia kuhusu VAR kwa kuwa matokeo yameshatokea na hayawezi kubadilika kwa namna yoyote.

“Unaweza kusema kwamba ilikuwa ni VAR lakini katika lipi sasa waweza kusema hivyo na nini ambacho kitatokea ilikuwa Dar na sasa ikawa Afrika ya Kusini.

“Ambacho kimetokea huwezi kukibadili kikubwa ni kuona kwamba tunaangalia mashindano yajayo kwenye mechi zetu zijazo,” amesema.

Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Yanga ambao ni wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 30,2022.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleSIKU YA MALARIA DUNIANI IMEWAKUTANISHA MERIDIANBET NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA AMANA