
KUMBE YANGA BADO INAJITAFUTA
BAADA ya Yanga kujikusanyia pointi 15 katika michezo mitano ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu huu, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amewataka mashabiki wao wasiwe na hofu kwani huu ni mwanzo tu, mazuri zaidi yanakuja. Yanga imekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo imefanikiwa kuweka rekodi ya kushinda mechi tano za mwanzo kwenye Ligi Kuu Bara kitu ambacho timu zingine zimeshindwa kufanya. Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alifichua kwamba, alitumia muda mrefu kuitengeza…