Home International GUARDIOLA: KDB ANAFURAHIA KUFUNGA

GUARDIOLA: KDB ANAFURAHIA KUFUNGA

PEP Guardiola,Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa ni lazima nyota wake Kevin De Bruyne,(KDB) awe kwenye furaha kubwa kutokana na kutumia uwezo wake kufunga mabao kila anapopata nafasi.

Kevin De Bruyne alitupia mabao 4 mbele ya Wolves wakati timu hiyo ikishinda mabao 5-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na kuweza kusepa na pointi tatu muhimu.

Ilikuwa ni dakika ya 7,16,24 na 60 huku lile bao la tano likipachikwa na Raheem Sterling dakika ya 84 kwa upande wa wenyeji Wolves wao walipata bao dakika ya 11 kupitia kwa Leander Dendoncker dk ya 11.

Ushindi huo unaifanya City kufikisha jumla ya pointi 89 ikiwa nafasi ya kwanza tofauti ya pointi tatu na wale waliopo nafasi ya pili ambao ni Liverpool wakiwa na pointi 86 na wote wamecheza mechi 36.

Pep amesema:”Nadhani sasa KDB anapenda kufunga kwa kuwa zamani alikuwa anapenda kutoa pasi ila ile tabia ya kufuatwa na wenzake wakati wa kushangilia na kumzunguka kwa furaha imeaanza kumzoea na yeye anapenda hivyo ni wakati wake wa kuendelea kufanya kile anachokipenda,”

Mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Molineux unawafanya mabingwa hao watetezi wazidi kukaribia lengo la kutetea taji lao.

Previous articleVIDEO:YANGA YAFUNGUKIA ISHU YA PENALTI YA MAYELE
Next articlePABLO:KIPINDI CHA PILI NILIKUJA NA MBINU TOFAUTI