Home International ISHU YA TAMMY KURUDI ENGLAND NGOMA NZITO

ISHU YA TAMMY KURUDI ENGLAND NGOMA NZITO

ROME, ITALY - SEPTEMBER 23: Tammy Abraham of AS Roma celebrates after scoring goal 1-0 during the Serie A match between AS Roma v Udinese Calcio at Stadio Olimpico on September 23, 2021 in Rome, Italy. (Photo by Silvia Lore/Getty Images)

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa kikosi cha AS Roma, Tammy Abraham yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi cha Arsenal kinachoshiriki Ligi Kuu England huku bosi wake akiweka wazi kwamba hadhani kama anaweza kurudi huko.

Roma ilimsajili Tammy msimu uliopita akitokea Chelsea na ilikuwa ni baada ya Kocha Mkuu Jose Mourinho kujiunga na timu hiyo.

Ni kwa mara ya kwanza Tammy amecheza ndani ya Serie A na amekuwa kwenye mwendo mzuri na kufanya kazi yake ya kucheka na nyavu akiwa ametupia mabao 25 katika michuano yote huku kwenye ligi akiwa amefunga mabao 15.

Mourinho amesema:”Alichagua na hii ni baada ya kuniamini mimi lakini sasa kama anataka kurudi England sidhani kama atafanya hivyo na kama anataka kurudi basi tutajua baadaye,”

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMIS
Next articleISHU YA MORRISON KUIBUKIA YANGA,SIMBA WATOA TAMKO